Share to:

 

A Fistful of Dollars

A Fistful of Dollars
(Per un pugno di dollari)
Imeongozwa na Sergio Leone
Imetayarishwa na Arrigo Colombo
Giorgio Papi
Imetungwa na Story:
A. Bonzzoni
Víctor Andrés Catena
Sergio Leone
Screenplay:
Victor Andrés Catena
Jamie Comas Gil
Sergio Leone
Nyota Clint Eastwood
Marianne Koch
Gian Maria Volonté
José Calvo
Joseph Egger
Antonio Prieto
Mario Brega
Wolfgang Lukschy
Sieghardt Rupp
Benny Reeves
Muziki na Ennio Morricone
Imesambazwa na United Artists
Unidis
Imetolewa tar. Italia:
16 Oktoba 1964
Marekani:
18 Januari 1967
Ina muda wa dk. Dakika 100
Nchi Italia
Hispania
Lugha Kiitalia
Bajeti ya filamu $200,000 (est.)
Ikafuatiwa na For a Few Dollars More

A Fistful of Dollars (kwa Kiitalia: Per un pugno di dollari}}) ni filamu ya Spaghetti Western ambayo ni ya Kiitalia-Kihispania. Filamu ilitolewa mnamo mwaka wa 1964. Filamu imeongozwa na Sergio Leone na ndani anakuja Clint Eastwood akiwa na Gian Maria Volonté, Marianne Koch, Wolfgang Lukschy, Sieghardt Rupp, José Calvo, Antonio Prieto, na Joseph Egger.[1]Filamu ilitolewa nchini Italia kunako mwaka wa 1964 halafu baadaye nchini Marekani kunako 1967. Iliwezesha kuipa umaarufu mtindo wa filamu wa Spaghetti Western.

Filamu ilifuatiwa na For a Few Dollars More (1965) na The Good, the Bad and the Ugly (1966), nazo pia nyota ni Eastwood. Zote kwa pamoja, filamu zinafahamika sana kwa jina la "Dollars Trilogy" au "The Man With No Name Trilogy". Filamu hii ni tengenezo la pili lisilo-rasmi la filamu ya Akira Kurosawa Yojimbo (1961), ambayo yenyewe imejizolea umaarufu mapema katika mtindo wa Kiwestern. Huko nchini Marekani, kina United Artists wamefanya kampeni ya kutaja uhusika wa Eastwood kwenye filamu zote tatu kama "Man with No Name".

Ikiwa kama filamu ya kwanza ya Spaghetti Westerns kutolewa nchini Marekani, washiriki wengi na wanakundi wa Kiulaya wamechukua majina yanayosika kuwa na asili ya Kimarekani. Hii ikiwa ni pamoja na Leone mwenyewe ("Bob Robertson"), Gian Maria Volonté ("Johnny Wels"), na mtunzi Ennio Morricone ("Dan Savio").

A Fistful of Dollars ilipigwa picha nchini Hispania, hasa walipiga karibia na Hoyo de Manzanares[2] inapakana na Madrid, lakini pia (kama jinsi zenzake mbili zilizofuatas) walipiga katika Hifadhi ya Taifa ya Cabo de Gata-Níjar katika Mkoa wa Almería.

Hadithi

Stranger (Clint Eastwood), anawasili katika mji mdogo wa mpakani mwa Mexiko, San Miguel. Mwenye hoteli, Silvanito (José Calvo), anamweleza Stranger kuhusu mtiti baina ya familia mbili zinagombania kushika hatamu ya mji huo: kwa upande mmoja, kina Rojo, ambapo inamwunganisha Don Miguel (Antonio Prieto) (mkubwa kumri na mkuu wa kazi), Esteban (Sieghardt Rupp) (kichwa ngumu), na Ramón (na mwenye uwezo wa kufanya lolote na vilevile ana akili sana, -mechezwa na Gian Maria Volonté); kwa upande mwingine, familia ya shariff wa mjini hapo, John Baxter (Wolfgang Lukschy).

Stranger, Joe (Eastwood), akiwa na mmili wa hoteli Silvanito (José Calvo), wakitazama wanajeshi wa Kimexiko wakiingiza mzigo wa dhahabu kupitia San Miguel.

Stranger, anatafuta njia ya kujiingizia kipato kutokana na hali iliyopo, ana-amua kuzichezea familia zote mbili ili zichukiane. Fursa hiyo kaipata pindi kundi la askari wa Kimexiko wakisindikiza mzigo wao wa dhahabu kupitia mjini hapo.

Kwa bahati mbaya au nzuri mzigo umefikishwa kwa kikosi cha jeshi cha Kimarekani kwa kubadilishana kwa silaha, lakini kwa kufuatia kutokuwepo kwa kikosi cha jeshi la Kimexiko mjini pale, Stranger alishuhudia watu wale wakiangamizwa na wanachama wa kikundi cha majambazi cha Rojo, wamevaa sare za Kimarekani huku wakiongozwa na Ramon Rojo. Kina Rojo wameutwaa mzigo wa dhahabu.

Stranger amechukua miili miwili na kuipeleka makaburi ya karibu na kuuza taarifa zile sehemu zote mbili kwamba askari wa Kimexiko wameponyeka katika shambulio. Pande zote mbili zimekimbilia makaburini kwa kasi ya ajabu, kina Baxter kwenda kuwachukua "wasaliaji" na kutoa ushahidi dhidi ya kina Rojo, kina Rojo, kwa lengo la kuwazima. Ugomvi huo ulipelekea kuleta mapambano ya bunduki, huku Ramon akifaulu "kuua" "wasaliaji" na Esteban kumteka mtoto wa John Baxter, Antonio.

Wakati kina Rojo na Baxters wanapigana, yule Stranger anatafuta dhahabu kwenye nyumba ya kina Rojo, lakini kwa bahati mbaya akagongana na mfungwa mrembo na bibi wa kilazima wa Ramón, Marisol (Marianne Koch), alipomshangaza. Kamchukua dada yule hadi kwa kina Baxter, ambaye amepanga amrudishe kwa kina Rojo ilimradi wabadilishane kwa Antonio.

Wakati wa kubadilishana, yule Stranger anatambua historia ya Marisol kutoka kwa Silvanito: "... familia ndogo yenye-furaha hadi hapo tabu ilipo-wakumba. Na hiyo shida ni jina la Ramon, akidai kwamba mumewe kamtapeli kwenye karata, ambapo ilikuwa si kweli. Hapo ndipo alipomchukua mke wa jamaa na kuishi naye kama teka."Usiku mmoja, wakati kina Rojo wanasherekea, yule Stranger kanyata na kumfungulia Marisol, piga risasi walinzi na kaharibu-haribu nyumba na kamtia kizuizini dada ilimradi ionekane kama vile lile shambulio limefanywa na kina Baxter.

Yule Stranger anamwambia Marisol, mume wake, na mtoto wao waondoke mjini pale, wakati huohuo anawapatia hela zitakazo wasaidia. Marisol anamuuliza yule Stranger, "Kwanini unatufanyia hivi?", na kwa mara ya kwanza na ya mwisho-pekee kwa Stranger kutoa kuonyesha matendo ya kibinadamu: "Kwanini? Kwa sababu awali kuna mtu nilikuwa nina mfahamu ambaye alikuwa kama wewe. Kulikuwa hakuna mtu wa kutoa msaada. Haya sasa mwende zetu".

Jamaa wakagundua kama amemtorosha Marisol, kina Rojo wakamteka yule Stranger na kumtandika, lakini alitoroka, kwa kumwua Chico (Mario Brega) wakati yu-mchakatoni kimateso. Wao wanaamini kwamba yule Stranger analindwa na kina Baxter, kina Rojo waka-washa moto nyumbani kwa kina Baxter na kuangamiza wale wote wanaojaribu kutoroka kutoka ndani. Miongoni mwa wafu wale ni pamoja na John Baxter, mke wake, Consuelo (Margarita Lozano), na Antonio. Sasa muhuni aliyebakia ni mmoja tu mjini San Miguel, kina Rojo wanamvamia Silvanito na kumpiga ile mbaya, ambaye wanamfikiria kwamba anamficha Stranger.

Yule Stranger anarudi mjini, ambapo anawakuta kina Rojo wapo katika hali ya shari. Akiwa na sahani la chuma alilolificha ndani ya nguo ya kifuani kwake, ana-wafanyia mzaha kina Ramon "wamlenge katika moyo" huku bunduki ya Ramon ina-dunda. Kaua wote kwa wakati mmoja pale kasoro Ramon, yule Stranger anatoa changamoto kwa Ramon ajaze bunduki yake haraka kuliko vile anavyofanya yeye, yule Stranger, anaweza kujaza pisto yake. Halafu kamndika na kumwua Ramon. Esteban Rojo, ambaye hakuonekana na Stranger na kumlenga kutoka katika jengo la karibuni, lakini alitandikwa risasi na kuuawa na Silvanito. Yule Stranger anaaga na kuanza safari ya kuondoka mjini pale.

Washiriki

Marejeo

  1. Variety film review; 18 Novemba 1964, page 22.
  2. "Los primeros decorados del Oeste en España, en Hoyo de Manzanares". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-01-08. Iliwekwa mnamo 2010-11-18.

Viungo vya Nje

Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu:
Index: pl ar de en es fr it arz nl ja pt ceb sv uk vi war zh ru af ast az bg zh-min-nan bn be ca cs cy da et el eo eu fa gl ko hi hr id he ka la lv lt hu mk ms min no nn ce uz kk ro simple sk sl sr sh fi ta tt th tg azb tr ur zh-yue hy my ace als am an hyw ban bjn map-bms ba be-tarask bcl bpy bar bs br cv nv eml hif fo fy ga gd gu hak ha hsb io ig ilo ia ie os is jv kn ht ku ckb ky mrj lb lij li lmo mai mg ml zh-classical mr xmf mzn cdo mn nap new ne frr oc mhr or as pa pnb ps pms nds crh qu sa sah sco sq scn si sd szl su sw tl shn te bug vec vo wa wuu yi yo diq bat-smg zu lad kbd ang smn ab roa-rup frp arc gn av ay bh bi bo bxr cbk-zam co za dag ary se pdc dv dsb myv ext fur gv gag inh ki glk gan guw xal haw rw kbp pam csb kw km kv koi kg gom ks gcr lo lbe ltg lez nia ln jbo lg mt mi tw mwl mdf mnw nqo fj nah na nds-nl nrm nov om pi pag pap pfl pcd krc kaa ksh rm rue sm sat sc trv stq nso sn cu so srn kab roa-tara tet tpi to chr tum tk tyv udm ug vep fiu-vro vls wo xh zea ty ak bm ch ny ee ff got iu ik kl mad cr pih ami pwn pnt dz rmy rn sg st tn ss ti din chy ts kcg ve 
Prefix: a b c d e f g h i j k l m n o p q r s t u v w x y z 0 1 2 3 4 5 6 7 8 9 
Kembali kehalaman sebelumnya