A New Day ...A New Day ... ilikuwa aina ya sanaa za nyimbo zilizoimbwa na Céline Dion katika ukumbi wa viti 4000 iliyopo Caesars Palace mjini Las Vegas. [1] Iliundwa na kuongozwa na Franco Dragone (anayojulikana kwa kazi yake kwa Cirque du Soleil na ikaanza tarehe 25 Machi 2003. A New Day ... ilianzisha mfumo mpya wa maonyesho ya burudani, kwa kuchanganya nyimbo, utendaji sanaa, ubunifu, na teknolojia. Ilichukua muda wa dakika 90. Dion alipewa mkataba wa miaka mitatu hapo awali, lakini kwa ajili ya mafanikio yake, yeye aliendelea kuimba kwa miaka miwili zaidi. A New Day ... ilimalizika 15 Desemba 2007, baada ya kuimbia kwa muda wa miaka 5 iliyo na zaidi ya maonyesho 700 na watazamaji milioni 3. Ilipata zaidi ya $400,000,000 kutoka maonyesho yote kwa jumla. [2] Kuhusu onyeshoChanzo cha onyesho hili lilitokea wakati Dion na mumewe René Angélil walitembelea Las Vegas mwaka 2000, pindi walipochukua mapumziko kwa ajili ya kuanza familia, walienda kuangalia O ya Cirque du Soleil katika Bellagio. Dion alifurahishwa na O na akasisitiza baadaye kupata kujua onyesho hili. Franco Dragone kwa upande wake, akasikia kuhusu furaha ya Dion kwa ajili ya kazi yake, na wiki kadhaa baadaye, aliwaandikia barua kutoa maoni yake kuhusu uwezo wa mashirikiano baina yake na Dion. Angelil alimwita Dragone, na katika mkutano wao A New Day ... ndiyo ilikuwa matokeo yake. Dion hapo awali alitaka onyesho lake liitwe Muse, lakini bendi yenye jina hil lilimiliki haki zake. Dion alitaka kuwapatia $50,000 kwa ajili ya haki hizo, lakini bendi hiyo ikakataa, mwimbaji mkuu wa bendi hiyo Matthew Bellamy akielezea kuwa hakutaka watu wafikiri kuwa wao ni wasaidizi wa Céline Dion. [3] Ukumbi huo ulijengwa kwa takriban siku 140. Steji ilipandishwa kidogo ili watazamaji wapate kunufaika vizuri. Madhumuni mengine ya kupandisha steji ni kwa ajili ya kuonyesha taa, miundo, na vitu vitakavyotumika kwenye onyesho hilo. Hii iliwasumbua miili ya wachezaji, na kusababisha wachache kuondoka kwenye onyesho hili kwa ajili ya majeraha waliopata. Mpango wa awali ulikuwa ni kutumia projekta, lakini wakati fundi, Yves Aucoin, alisema kuwa hii ingeleta vivuli wakati wachezaji wanakimbia mbele yake; Angelil akamshawishi Phil Anschutz, achangie dola milioni 10 zaidi kwa ajili ya ujenzi wa skrini ya LED. LED ilitayarishwa na Mitsubishi Diamond Vision LED Screens. Hii ilikuwa LED Screen HDTV iliyo na 8mm Display "Dot Pitch". Ilikuwa ni skrini nyingi zimewekwa pamoja. [4] Orodha ya nyimbo
Mengineyo
Matukio
Maonyesho na rekodiTarehe ya kutoa DVD ilibadilishwa kutokana na mabadiliko ya nyimbo. Badala yake, CD ilitolewa mnamo Juni 2004. [5]A New Day ... ilirekodiwa mnamo 17-21 Januari2007 na ikatolewa katika DVD tarehe 7 Desemba 2007 na kwenye Blu-ray Disc tarehe 5 Februari 2008. [6] Ilikuwemo: onyesho lenyewe, na Because You Loved Me (A Tribute to the Fans), A New Day: All Access na A New Day: the Secrets, ilifanikiwa kwenye chati kote duniani. [7] Wafanyikazi
Bendi
Tuzo
Marejeo
|