Age Ain't Nothing But a Number
Age Ain't Nothing but a Number ni albamu ya kwanza ya msanii wa rekodi za muziki wa R&B kutoka nchini Marekani, Aaliyah. Albamu ilitolewa chini ya studio ya Jive na Blackground Records mnamo tar. 13 Juni 1994, huko nchini Marekani. Baada ya kuingia mkataba na mjomba'ke Barry Hankerson, Aaliyah akatambulishwa kwa msanii na mtayarishaji wa rekodi R. Kelly. Akawa mshauri na mtu wake wa karibu, vilevile akiwa kama mtunzi na mtayarishaji mkuu wa albamu hii. Wawili hao wamerekodi albamu katika Chicago Recording Company huko mjini Chicago, Illinois. Albamu imetoa vibao vikali viwili, ikiwa ni pamoja na kupata chati katika kumi bora kwa kibao cha "Back & Forth" na "At Your Best (You Are Love)"; single zote mbili zilitunukiwa Dhahabu na Recording Industry Association of America (RIAA). Single mbili za ziadi zilifuata: "Age Ain't Nothing But a Number" na "No One Knows How to Love Me Quite Like You Do". Age Ain't Nothing But a Number imepokea tahakiki za kiupendeleo na haki kutoka kwa watalaamu wa uhakiki. Albamu iliingia nafasi ya 18 kwenye chati za Billboard 200 na kuuza nakala milioni tatu kwa nchini Marekani, ambapo ilipata kutunukiwa platinamu mara mbili na RIAA mnao tar. 24 Oktoba 2001. Orodha ya nyimboNyimbo zote zimetungwa na R. Kelly, kasoro zile zilizowekewa maelezo.
Chati
Tanbihi
Marejeo
|