Autobiography of a GeishaAutobiography of a Geisha (芸者―苦闘の半生涯 Geisha, kutō no hanshōgai ) ni kitabu kilichoandikwa na Sayo Masuda (増田 小夜 Masuda Sayo ). Kuhusu TawasifuMasada alikuwa geisha (mwanamke mtumbuizaji wa Kijapani aliye na uwezo wa kufanya sarakasi nyingi za muziki na kukatika) aliyekuwa akiishi katika kijito cha maji-moto nchini Japan. Alizaliwa mnamo 1925 karibu na mji wa Shiojiri kule Nagano Prefecture. Masuda aliiandika tawasifu yake kati ya mwaka wa 1956 na 1957. Kutokana na ukosefu wake wa kusoma vitabu, Masuda alikuwa na umahiri kidogo sana wa kifasihi, kwa hivyo aliiandika tawasifu yake kwa lugha ya hiragana, aina ya nukta rahisi zaidi za Kijapani. Wahariri wake walijaribu wawezavyo kuitafsiri tawasifu hiyo na kuipanga bila kupoteza ladha ya uandishi wa asili. Yaliyomo katika Tawasifu hiyoAkiwa motto, Masuda alikuwa akiishia na mlezi katika shamba kubwa la nyumbami ambapo hakupata chakula cha kutosha, hakupata elimu wala makazi mema na alikuwa akiadhibiwa mara kwa mara. Alipokuwa umri wa miaka 12, mamake alihitaji fedha za kulipia matibabu ya mumewe. Mjomba wake alimtafuta shambani na kumuuza kwa jumba la watumbuizaji/geisha (okiya) lililoitwa Takenoya. Wakati huo jina lake la utani likawa ‘’Crane’’ kwa sababu hakuruhusiwa kuvaa soksi na angeinua mguu wake mmoja na kuupa joto wayo wake kwa paja la mguu mwingine. Jina hili la utani lilitumiwa hata baada ya kuhamia ‘’okiya’’. Hakuwa anajua jina lake halisi hadi alipopelekwa hospitalini kw matibabu baada ya kujiumiza akitumbuiza kama geisha na madaktari wakamwita ‘’’Bi. Masuda’’’. Tawasifu ya Masuda inaelezea kwa undani kuhusu jitihada zake kama geisha katika bustani ya kijito cha maji ya moto. Watumbuizaji hawa walihitajika kutenda ngono na wateja wao, jambo lililomfanya Masuda kujiamulia kuwa mbinu ya pekee aliyokuwa nayo katika maisha ilikuwa kuuza mwili wake. Alijaribu katika maisha yake yote kupingana na fikira hii. Vitabu vyake vinasimulia wakati wake kama geisha, jitihada zake kuingia nchini Japan, jitihada za kuiweka pamoja familia yake iliyosambaratika na tama yake ya kutoka katika biashara ya ngono kabisa. Masuda alitamani kupata elimu na kupata ajira ya maana, mambo ambayo takribani yasingewezekana kufuatia familia yake iliyokudharauliwa na wengi. Katika tawasifu yake Masuda anasisitiza umuhimu wa wazazi kuhusikana na watoto wao na wasizae watoto ambao hawako tayari kuwalea. Masuda hakuolewa wala kuzaa mtoto lakini njia bora ya kuupitisha wakati wake ilikuwa kuwalea watoto wa wengine. Kitabu cha Masuda ‘’Autobiography of a Geisha’’, kwa mshangao, kimedharauliwa katika uchapishaji kuhusu ‘’geisha’’. Katika tawasifu yake ya Geisha, a Life (Pia iitwayo Geisha of Gion), Mineko Iwasaki anadai kuwa geisha wa kwanza kujitokeza kusimulia historia yake na wasomi wengi huunga madai haya mkono, iingawa kazi ya Masuda ilichapishwa kitambo kabla ya ile ya Iwasaki. Orodha ya WahusikaTakemi, Shizuka, Karuta, Takechiyo: Masuda’s older sisters in the Okiya Tsukiko: One Mmoja wa dada zake wadogo kule Okiya Mama: Mamake Masuda wa Kiokiya, mtoa adhabu kali Cockeye: Danna wa kwanza wa Masuda, mdhamini wa muda mfupi, kiongozi wa kundi la kijangili, na anayependelea sana mabikira Hii-san: aliyekuwa mpenzi wa Tsukiko, mwana wa mwenye kiwanda kidogo kule Suwa. Naoko: Hawala wa kwanza wa Cockeye. Alikuwa na mkahawa katika mji wa Lower Suwa. Motoyama-san: Mwana wa mwanabiashara wa pombe. Alikuwa msaidizi wake wa pili, akawa mgonjwa na kuachiliwa kwa muda kutoka huduma ya kijeshi. Alikuwa akifanya kazi katika Nippon Wireless Kaka: Mmoja wa kaka zake. Amejitolea kwa Masuda, he suffered Aliugua ugonjwa wa Kifua Kikuu wa matumbo na akajiua katika hospitali. Marejeo
New York : Columbia University Press, 2003. ISBN 0231129513 |