DaxibotulinumtoxinADaxibotulinumtoxinA, inayouzwa kwa jina la chapa Daxxify, ni dawa inayotumika kuboresha mwonekano wa mikunjo inayopatikana kati ya nyusi. [1] Inaweza pia kutolewa kwa ajili ya kutibu ugonjwa sugu wa neva unaosababisha shingo kugeukia kushoto, kulia, juu, na/au chini bila hiari (cervical dystonia).[2] Dawa hii inatolewa kwa njia ya kudunga sindano kwenye misuli.[1] Madhara yake yanaweza kudumu kwa hadi miezi sita.[2] Madhara yake ya kawaida ni pamoja na maumivu ya kichwa, kuanguka kwa kope na shida ya kusonga uso.[1] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha matatizo ya kumeza au kupumua.[1] Ni sumu ya botulinamu A (botulinum toxin A) ambayo huzuia kutolewa kwa asetilikolini (acetylcholine) na ni ajenti ya kuzuia neva za fahamu (neuromuscular blocking agent).[1] DaxibotulinumtoxinA iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 2022.[1] Ni mshindani wa kibiashara kwa Botox.[3] Marejeo
|