Love Don't Cost a Thing
"Love Don't Cost a Thing" ni single kiongozi kutoka kwa albamu ya Jennifer Lopez inayoitwa J.Lo (2001). Ilikuwa namba 3 kwenye chati ya Billboard Hot 100, kando ya kuwa namba 1 nchini Uingereza. Lopez aliimba nyimbo hii kwa mara ya kwanza kwenye sherehe za MTV Europe Music Awards 2000 mnamo Novemba 2000, mjini Stockholm, Sweden. VideoVideo ya wimbo hii inaanza pale Lopez anaongea na mpenzi wake kwa simu; akimwambia Lopez kuwa hatoweza kuja. Kisha, anamuuliza Lopez ikiwa amepata bangili aliyomletea, na Lopez anamjibu kuwa angefurahia ikiwa yeye angekuja, badala ya kumnunulia bangili, kisha Lopez akakata simu kwa hasira. Kisha, Lopez anatoka kwa jumba aliyokuwemo, na kuingia kwenye gari na akaelekea baharini. Alipofika, alivua miwani na koti lake na kutoa barua iliyoandikwa: "Natamani ungelikuwa nami". Lopez anaendelea kuimba kando ya bahari na mwishowe, anatoa fulana aliyovaa na kufinika matiti yake kwa mikono yake. Video hii ilipigiwa kura kwenye sherehe za 2001 MTV Video Music Awards: Best Female Video na Best Dance Video. ChatiNchini Marekani, "Love Don't Cost a Thing" ilikuwa kwenye chati ya Billboard Hot 100 namba 46, mnamo 9 Desemba 2000. Wiki tatu baadaye, single hii ilikuwa kwenye top 20, na kisha ikapanda kutoka namba 10 hadi 4, mnamo 27 Januari 2001. "Love Don't Cost a Thing" ilibaki kwa namba 3 kwa muda ya wiki mbili mfululizo. Nchini Asia, wimbo hii ilikaa kwenye chati ya MTV Asia Hitlist kwa muda ya wiki saba. Orodha
Chati"Love Don't Cost a Thing"
Thibitisho
Marejeo
|