Guadeloupe![]()
![]() Guadeloupe ni eneo la ng'ambo na mkoa (departement) wa Ufaransa katika Bahari ya Karibi lenye visiwa tisa vidogo. Hivyo ni sehemu ya Umoja wa Ulaya. Makao makuu ni Basse-Terre, ingawa mji mkubwa ni Pointe-à-Pitre. Wakazi asilia walikuwa Waindio. Utamaduni wao uliharibiwa kabisa kwa kuja kwa ukoloni kutoka Ulaya (1493). Ilikuwa koloni la Ufaransa halafu la Uingereza halafu la Uswidi halafu la Ufaransa tena. Eneo lake ni km² 1,628. WatuIdadi ya wakazi ni 394,110. Asilimia 71 za wakazi ni wa asili ya Afrika au machotara. Wazee wao waliletwa huko kama watumwa kwa ajili ya kazi za mashamba ya miwa. 15% ni Wahindi, 9% Wazungu, 3% Wachina na 2% Waarabu. Lugha rasmi ni Kifaransa, lakini wengi wanaongea pia Krioli. Upande wa dini, 80% ni Wakatoliki na 5% Waprotestanti. Tazama pia
Viungo vya nje
Serikali
Safari
|