Japani
Japani ni nchi ya visiwa katika Pasifiki, mkabala wa mwambao wa mashariki ya Asia. Wajapani wenyewe hutumia jina la "Nihon" au "Nippon" lenye maana ya "Mwanzo wa jua". Hivyo Japani huitwa pia "Nchi ya Macheo". Nchi ina eneo la km² 377.944; na wakazi milioni 127; idadi hiyo imeanza kupungua. Japani ni kati ya nchi za dunia zilizoendelea sana upande wa sayansi, teknolojia na uchumi. Ilikuwa nchi ya kwanza nje ya Ulaya iliyofaulu kujenga jamii ya viwanda. JiografiaJapani ni funguvisiwa lenye visiwa 14,125 mbele ya pwani ya Uchina, Korea na Urusi (Siberia). Visiwa vikubwa na muhimu zaidi ni vinne tu; ndivyo Honshu, Hokkaido, Shikoku na Kyushu. Safu ya milima inapita visiwa vyote vikubwa na kusababisha msongamano mkubwa wa wakazi katika miji kutokana na uhaba wa ardhi ya kukalia. Hali halisi Japani yote ni safu ya milima tu inayopanda juu kutoka sakafu ya bahari na vilele vya milima yake huonekana juu ya uso wa bahari kama visiwa vikubwa au vidogo. Kijiolojia eneo hili liko kwenye mstari ambako mabamba ya gandunia ya Ulaya-Asia, Pasifiki na Ufilipino hukutana. Hii ni sababu ya kuwepo kwa volkeno 240 katika Japani na takriban 40 kati ya hizo ni hai pia kutokea kwa matetemeko ya ardhi ya mara kwa mara. Hivyo Japani ni sehemu ya pete ya moto ya Pasifiki inayozunguka bamba la Pasifiki. Japani inapatwa kila mwaka na dhoruba kali aina ya taifuni. Hata tsunami (ni neno la Kijapani) ni kawaida. Nchi inajikinga na mitambo mengi ya kutoa taarifa ya tsunami kuanza pia mitambo ya kufunga milango ya mabandari. MijiWajapani wengi hukalia sehemu ndogo ya 10% za nchi. Kuna miji kumi yenye wakazi zaidi ya milioni moja. Miji mikubwa ni Tokyo, Yokohama, Nagoya, Osaka, Kyoto, Kobe, Hiroshima, Fukuoka, Kitakyushu, Sendai na Sapporo. Usafiri ndani ya Japani ni hasa kwa treni, mabasi na ndege. Treni ya Shinkansen visiwani Honshu na Kyushu ni kati ya treni zenye mkasi mkubwa duniani. MikoaJapan ina mikoa arubaini na saba. Kila mkoa unasimamiwa na gavana mmoja, bunge na urasimu utawala. Kila mkoa umegawanyika katika miji na vijiji.
Kwa sasa manispaa za Japani zinaundwa upya kwa kuunganisha mikoa, miji na baadhi ya vijiji. Mabadiliko hayo yatapunguza idadi ya miji nchini Japani.[1] HistoriaVisiwa vilikaliwa na binadamu tangu miaka 30,000 KK. Wakazi wa sasa wametokana na mchanganyiko wa makabila asili (kama Waainu) na Wakorea waliovamia visiwa hivyo. UchumiJapani ni nchi ya tatu duniani kwa ukubwa wa uchumi. Utamadunini vyakula kama vile kobe,jongoo, na mbpga za majani....pia njia za kiasili za kuabudu kama kwenye matempo mbalimbali DiniWajapani wanaweza kushiriki ibada za dini mbalimbali kadiri wanavyojisikia, lakini asilimia 60 hawana dini maalumu. Wabuddha ni asilimia 34, wafuasi wa madhehebu ya Shinto ni asilimia 4, Wakristo sanasana ni asilimia 2.3. Tazama piaTanbihi
Marejeo
Viungo vya nje
|