Kupro
Kupro (pia: Kipro, Kuprosi, na hata Saiprasi kutoka Kiingereza Cyprus) ni nchi ya kisiwani upande wa mashariki wa bahari ya Mediteranea. Kijiografia ni sehemu ya Asia, lakini kiutamaduni na kisiasa ni sehemu ya Ulaya. HistoriaKisiwa cha shabaWatu waliishi huko walau kuanzia milenia ya 10 KK. Zamani za Kale kisiwa kilikuwa chanzo cha shaba nyingi iliyopatikana katika eneo la Mediteranea ya mashariki. Jina la kikemia la shaba "kupri" linatokana na jina la kisiwa hicho. Katika BibliaKisiwa kinazungumziwa na Biblia ya Kikristo, kwa namna ya pekee kuhusiana na umisionari wa Mtume Barnaba na wenzie Mtume Paulo na Marko Mwinjili kisiwani huko. Kuanzia mwaka 649 Kupro ilishambuliwa na pengine kutawaliwa na Waarabu walioua wakazi wengi na kubomoa makanisa na miji mizima. Chini ya WaosmaniBaada ya Wakristo kujirudishia kisiwa hicho muhimu, Waturuki Waosmani walikiteka mwaka 1570 na kuingiza Uislamu bila kufaulu kufuta dini ya awali. Chini ya WaingerezaMwaka 1878 Uingereza ulianza kutawala Kupro bila kuitenga rasmi na Dola la Waosmani hadi mwaka 1914. UhuruTarehe 16 Agosti 1960 Kupro ilijipatia uhuru ingawa kulikuwa na utata kati ya kubaki peke yake, kuungana na Ugiriki au kugawiwa kati ya kaskazini (Waturuki) na kusini (Wagiriki). Baada ya uhuruTangu vita vya Kupro, 1974 kisiwa kimegawiwa, huku maeneo ya kaskazini yakiwa yanatawaliwa na Jamhuri ya Kituruki ya Cyprus ya Kaskazini isiyotambulika kimataifa. Pamoja na hayo, Kupro imefaulu kujiunga na Umoja wa Ulaya tarehe 1 Mei 2004. WatuWakazi walio wengi hutumia lugha ya Kigiriki, wengine Kituruki, ambazo zote mbili ni lugha rasmi. Kwa jumla hao wa kwanza ni Wakristo (72.3% za wakazi wote), wa pili ni Waislamu (25%). Wakristo karibu wote ni Waorthodoksi; wengine ni Wakatoliki (2.9%, hasa Wamaroni), Waprotestanti (2%) na Waarmenia. Dini ina nafasi kubwa katika maisha ya wananchi. Tazama piaViungo vya nje
|