Lyon
Lyon ndiyo mji mkuu wa mkoa wa Rhône-Alpes na wa tatu katika Ufaransa nzima. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka 2007, mji huu pamoja na vitongoji vyake una wakazi wapatao milioni 4.4. Mji upo mita 162-312 juu ya usawa wa bahari. Lyon katika historiaKihistoria ni muhimu tangu zamani, kwa kuwa ulikuwa mji mkuu wa Gallia. Kiini cha mji kimeorodheshwa na UNESCO mwaka 1998 katika Urithi wa dunia. Kutoka huko Ukristo ulienea katika nchi inayoitwa sasa Ufaransa. Ndiyo sababu askofu wake anahesabiwa mpaka leo kuwa mkuu kuliko wale wote wa nchi hiyo. Maarufu kati ya watakatifu wake: wafiadini wa Lyon na askofu Ireneo. Katika karne ya 13 mjini ilifanyika mitaguso miwili inayohesabiwa na Kanisa Katoliki kuwa mitaguso mikuu: Mtaguso I wa Lyon (1245) na Mtaguso II wa Lyon (1274). Mpaka leo jimbo hilo linadumisha mambo machache ya pekee katika liturujia kufuatana na mapokeo ya Gallia (Liturujia ya Lyon). Tazama piaViungo vya nje
Information related to Lyon |