ValdoPetro Valdo (kwa Kifaransa: Pierre Vaudès/de Vaux, 1140 hivi - 1179 au 1205 hivi), anatajwa kwa mwanzilishi wa Wavaldo, tapo la Ukristo la Karne za Kati. MaishaHakuna habari nyingi za hakika kuhusu maisha yake. Mfanyabiashara wa Lyon, Ufaransa, aliongoka kwa kuacha mali yake na kushika ufukara[1][2][3]. Alianza pia kuhubiri, hasa kwamba, "Hakuna anayeweza kuyumikia mabwana wawili, Mungu na mali".[4] Kufikia mwaka 1170 Valdo alikuwa ameshapata wafuasi wengi walioiga maisha yake ya Kiinjili.[5] Anasifiwa pia kwa kutoa au kuagiza tafsiri ya kwanza ya Biblia katika lugha yoyote mpya iliyotokana na Kilatini.[6] Mwaka 1179, Valdo na mfuasi wake mmojawapo walikwenda Roma, walipokaribishwa na Papa Alexander III. Mwaka huohuo mtaguso wa tatu wa Laterano ulikataa baadhi ya mawazo ya Valdo, bila kulaani tapo lenyewe wala kutenga viongozi wake. Lakini itikio la maaskofu lilikuwa kali zaidi, hivyo Wavaldo walifukuzwa kutoka Lyon, na hatimaye walijitafutia usalama katika mabonde ya Piemonte, Italia Kaskazini.[7] Baada ya mwanzo wa Matengenezo ya Kiprotestanti, Wavaldo walijiunga nayo, hasa katika mfumo wa Wakalvini (1532).[8] Kwa sasa Wavaldo ni 70,000 hivi. Tanbihi
Marejeo
Viungo vya nje
|